Web

Lipumba: Tumeshajeruhiwa na Muungano wa Vyama Vya Upinzani.....

Lipumba: Tumeshajeruhiwa na Muungano wa Vyama Vya Upinzani.....


Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba, amesema kuwa maridhiano ndani ya vyama vya upinzani yamekuwa yakileta madhara na kuwajeruhi, na kwamba wamejifunza kutokana na yaliyotokea kipindi cha nyuma.


Akizungumza na Wanahabari Lipumba amesema kuwa kuna watu wanaotafuta madaraka kwa maslahi binafsi badala ya kujenga demokrasia ya kweli.


Amesema kuwa mwaka 2020, alikumbana na hali ya kushangaza ambapo alijitokeza kugombea urais, lakini alikumbana na pingamizi la dakika za mwisho kutoka kwa Tundu Lissu, jambo ambalo alidai lilikuwa kinyume na misingi ya demokrasia.


Lipumba amesema kuwa ingawa alikamilisha taratibu zote za kisheria, alikumbana na kikwazo cha kisiasa kilichotokana na Mpinzani mwenzake ambaye alikuwa Mgombea Urais wakati huo kupitia Chadema Tundu Lissu


"Sasa ukishajua kwamba umegongwa, umeumwa lazima uwe na tahadhari, kuna watu ambao wanatafuta madaraka sio kujenga demokrasia.wapo kama Trump kwamba ukishaingia basi uanze kuwashughulikia wote, lazima tuwe macho katika hili kwa sababu tushagongwa gangwa sana" amesema Lipumba.


Prof. Lipumba ameongeza kuwa katika historia ya siasa za upinzani, vyama vimekuwa vikishirikiana kwa makubaliano ya muda mfupi, lakini mara nyingi hayo yamevurugwa kutokana na kutokuwa na umoja wa kweli. Akirejelea uchaguzi wa 2014, alikumbusha jinsi baadhi ya vyama vilivyokuwa vikitumia udhaifu wa vyama vingine kujinufaisha.


Amesisitiza kuwa ili kuhakikisha demokrasia inakua nchini, vyama vya upinzani vinapaswa kuwa na maridhiano ya kweli na ya kudumu, badala ya kuingiza maslahi binafsi katika vikao vyao.


"Mifumo isiyo huru tulikubaliana kabisa sasa mnafanyeje pasina kuwa na maridhiano, sasa ukiwa unahitaji unatoa wito kwamba tufanye maridhiano, tufanye mazungumzo tukae katika kikao cha pamoja.sasa ikiwa ndo wito wako huo ukaweka tu kama hatukai kwenye kikao cha pamoja hili na hili, moja kwa moja unaonekana kwamba hauhitaji kuwa na maridhiano."


"Katika masuala ya kidiplomasia inabidi nondo zako zingine uziweke akiba.kama utakwenda na kauli mbiu kwamba tutaicheza ngoma kwa Kadri itakavyodundwa basi hiyo msitoe mapema iweke akiba.lakini pia uwaandae watu" amesisitiza Lipumba

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad