Web

M23 Wababe Sana, Wagoma Kusitisha VITA, Wateka Mji Mpya Kongo

Top Post Ad

M23 Wababe Sana, Wagoma Kusitisha VITA, Wateka Mji Mpya Kongo


Kundi la Waasi M23 limegoma kusitisha vita ambapo limeendelea ma mashambulizi mashariki mwa Kongo na kuingia katika Mji wa Walikale ikiwa zimepita siku mbili baada ya Rais wa Kongo Felix Tshisekedi na Rais wa Rwanda Paul Kagame watoe wito wa kusitisha mapigano kufuatia mkutano wao huko Qatar.

Milio ya risasi ilisikika usiku wa jana karibu na mji huo katika eneo la Nyabangi ambako mapigano yamekuwa yakiendelea kati ya Waasi wa M23 na jeshi la Kongo katika Mji huo wa Walikale wenye utajiri mkubwa wa madini unaopatikana takriban kilometa 125 kaskazini magharibi mwa Goma.

Waasi hao walikuwa wakipambana na Wanajeshi na Wanamgambo wanaoiunga mkono Serikali baada ya kuvuka eneo la jeshi nje ya Mji huo katika shambulio la kushtukiza, kusonga mbele kwa M23 upande wa magharibi kulilazimisha kampuni ya Alphamin Resources wiki iliyopita kusimamisha shughuli katika mgodi wake wa madini ya tin wa Bisie, takriban kilomita 60 kaskazini magharibi mwa mji wa Walikale.

Mji huo wenye takriban Watu 15,000 upo umbali wa kilomita 125 (maili 80) kaskazini-magharibi mwa mji mkubwa wa Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambao Waasi waliuteka mwezi January mwaka huu, na kuwaweka ndani ya kilomita 400 kutoka Kisangani Mji wa nne kwa ukubwa nchini Kongo.

Below Post Ad

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.