Web

Makamu wa Rais wa Yanga: Hakuna Tena Mechi ya Yanga na Simba, Imeisha Hiyo




Makamu wa Rais wa Yanga SC, Arafat Haji, ameweka wazi kuwa mechi ya watani wa jadi kati ya Yanga SC na Simba SC, iliyokuñwa imepangwa kufanyika Machi 8, 2025, haitapangiwa tarehe nyingine baada ya kuahirishwa.

Kupitia ujumbe wake kwenye Instagram, Arafat amewapongeza mashabiki wa Yanga kwa kujitokeza kwa wingi uwanjani kutoka maeneo mbalimbali nchini, akitambua juhudi zao za kusafiri kwa njia tofauti ili kushuhudia mchezo huo.

Amesisitiza kuwa viongozi wa Yanga walifanya kila wawezalo kuhakikisha timu inafika uwanjani tayari kwa mchezo huo, lakini hatimaye mechi haikufanyika. Akiwa na masikitiko makubwa, amewapa pole mashabiki kwa muda na fedha walizopoteza kwa ajili ya mechi hiyo, huku akisisitiza kuwa maumivu hayo ni ya kila mmoja ndani ya familia ya Yanga SC.

Arafat pia amewashukuru wachezaji na benchi la ufundi kwa heshima waliyoonyesha kwa mashabiki, akisema kuwa kufika kwao uwanjani ni ishara ya kujitolea kwa ajili ya nembo ya Kijani na Njano.

Kwa msisitizo mkubwa, amesema kuwa hakutakuwa na mechi nyingine ya ligi kati ya Yanga na Simba msimu huu wa 2024/25, na kwamba klabu sasa inaangazia michezo mingine kwenye ratiba yao.

Amehitimisha ujumbe wake kwa kuwatakia safari njema mashabiki waliokuwa wamefika uwanjani, akiwatakia baraka na ulinzi wanaporejea kwa familia zao.

“Daima Mbele, Nyuma Mwiko!” – Arafat Haji, Makamu wa Rais Yanga SC.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad