Serikali yaijia juu bodi ya ligi baada ya bodi ya ligi kutaka msaada kutoa serikalini na hii ni baada ya klabu ya yanga kudai alama tatu dhidi ya mpinzani wake simba lakini bodi ya ligi wameitupilia mbali hoja hiyo na hivyo imewataka wakae kikao na klabu ya yanga lakini klabu ya yanga awajataka kukaa kikao chochote kile na bodi ya ligi.
Aliyekua Msemaji wa Yanga amesema kuna uzushi unaendelea kuwa Serikali itaingia suala la Derby ya Kariakoo ambapo amesisitiza hata wao wameshabaini wenye mamlaka ya mpira wamekosea hivyo nao wamekaa pembeni hawataki kuchonganishwa na wananchi ikizingatiwa huu ni mwaka wa uchaguzi.
Kwamba Serikali haitaki kubeba mzigo wa mtu ,acha wahangaike nao wenyewe kwani serikali inajiandaa na msimu wa kampeni hivyo serikali haitaki kuingilia maswala kama hayo kwani ni jambo zito sana serikali kuingilia kati maswala ya kimchezo kwani sheria ya mpira aitaki serikali ijiusishe na maswala ya mpira kwani mpira utaongozwa na sheria na taratibu zake
Mpira wa Tanznia umekuwa na mpira wenye maendeleo makubwa sana hivyo basi chochote kinachofanyika ni kutia doa katika mpira huu kwani endapo serikali itaingilia kati maswala ya mpira litakuwa ni kosa kubwa na uenda ikasabisha ata Shirikisho la mpira duniani kuingilia kati
Bodi ya ligi wanatakiwa wajitathmini kwa hiki wanachokifanya kwani siyo kujenga mpira bali ni kubomoa na chanzo ya hayo yote ni baada y raisi wa mpira wa miguu Tanzania wallace karia kuongea maneno ambayo yalileta mijadala mingi sana mtandaoni kwani aikuwa sahihi kwa mtu kama yeye kuzungumza maneno kama yale siyo jambo zuri na alikustahili kuzungumzwa.