Web

Marekani Chini ya Utawala wa Trump Haita Ipa Tena Ukraine Msaada wa Kivita.....



Marekani chini ya utawala wa Rais Donald Trump imetangaza kuwa haitoendelea tena kuisaidia Ukraine kifedha wala silaha za kivita kwasababu kipaumbele cha Marekani ni majadiliano ya amani na kumaliza vita ya Ukraine na Urusi.

Uamuzi huu wa Marekani umetangazwa usiku wa kuamkia leo March 01,2025 na Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Caroline Leavitt ikiwa imepita siku moja tangu Trump na Rais wa Ukraine Zelensky wazozane mbele ya camera za Waandishi wa Habari.

Caroline amesema “Hatutoendelea tena kuandika check kufadhili vita, hatutoendelea kuifadhili nchi ambayo haitaki amani ya kudumu, ilikuwa vizuri kwamba camera zimeonesha ule mzozo wa Trump na Rais wa Ukraine na Wamarekani na Dunia nzima imeona kile ambacho Trump na Timu yake wanashughulika nacho nyuma ya pazia wakati wa majadiliano ya kumaliza vita”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad