Web

Marekani imemtimua Balozi wa Afrika Kusini




Marekani imemtimua Balozi wa Afrika Kusini mjini Washington Ebrahim Rasool akituhumiwa kuichukia Marekani na kumchukia Rais Donald Trump.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, amesema Marekani inamfukuza Balozi wa Ebrahim kwa kuichukia Marekani na Rais Donald Trump ambapo Rubio ameandika katika mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter) leo March 15,2025 kwamba Balozi huyo wa Afrika Kusini nchini Marekani hakaribishwi tena katika nchi yao na hawana la kujadili nae, hatua hii inakuja siku chache baada ya Balozi Rasool kusema Trump anaendesha vuguvugu la kuwafanya Watu weupe kuwa bora kuliko wengine nchini Marekani na Dunia nzima kwa ujumla.

Kufukuzwa kwa Balozi Rasool, hatua ya nadra kuchukuliwa na Marekani, ni tukio la hivi karibuni kabisa la ongezeko la msuguano kati ya Serikali ya Marekani na ile ya Afrika Kusini… Balozi Rasool ni Mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi tangu ujana wake na mara kadhaa ameelezea hasira zake kwa Serikali ya Israel kufanya vita Gaza.

Itakumbukwa Febraury mwaka huu Trump alisitisha msaada kwa nchi ya Afrika Kusini akitaja sababu kuwa ni sheria kali nchini Afrika Kusini ambayo anadai inaruhusu ardhi kutekwa kutoka kwa Wakulima weupe.

Wiki iliyopita Trump alichochea zaidi hali ya wasiwasi akisema Wakulima wa Afrika Kusini wanakaribishwa kwenda kuishi Marekani baada ya kurudia madai yake kwamba Serikali ya Afrika Kusini inachukua kwa nguvu ardhi kutoka kwa Watu weupe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad