Web

Mashujaa Watozwa Faini Milioni 5 Kisa Kufanya Uchawi Live Mechi na Yanga....




Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Machi 28, 2025 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya maamuzi yafuatayo kwenye baadhi ya michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara.



Mechi Namba 148: Simba SC 6-0 Dodoma Jiji FC

Timu ya Dodoma Jiji ya mkoani Dodoma imepewa Onyo Kali kwa kosa la kujumuïsha mchezaji mmoja pekee kutoka timu za vijana badala ya wawili, kwenye orodha ya wachezaji 21 kwa ajili ya mchezo tajwa hapo juu, kinyume na matakwa ya Kanuni ya 17:6(6.2) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo. Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 17:62 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Mechi Namba 166: Mashujaa FC 0-5 Young Africans SC

Klabu ya Mashujaa imeadhibiwa kwa kutozwa faini ya Sh. 5,000,000 (milioni tano) kwa kosa la wachezaji wake kuonekana wakifanya kitendo ambacho si cha kawaida na kilichohusishwa na imani za kishirikina ya kushuka kwenye basi lao, wachezaji wa klabu hiyo waligeuka na Baada kuanza kutembea kinyumenyume (wakitanguliza migongo) wakati wakiingia kwenye mlango wa kuelekea vyumba vya kuvalia. Adhabu hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 47:51 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Klabu.


Mechi Namba 172: JKT Tanzania 1-1 KenGold FC

Klabu ya KenGold ya mkoani Mbeya imeadhibiwa kwa kutozwa faini ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la kukataa kutumia chumba maalum cha kuvalia kwa kile walichoeleza kuwa kulikuwa na harufu mbaya kwenye choo cha chumba hicho. Hata hivyo, taarifa za maofisa wa mchezo huo zilieleza kuwa hakukuwa na harufu mbaya iliyoelezwa na maofisa wa klabu hiyo. Jambo hilo ni kosa kwa mujibu wa Kanuni ya 17:20 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo na adhabu hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 17:62 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Asante sana kwa kusoma makala hii ndugu msomaji nakuomba like pamoja na kutoa maoni yako hapo chini ya habari hii kisha ubonyeze kitufe kilichoandikwa Subscribe hapo juu ya habari hii ili uwe mtu wa kwanza kila siku kupata habari moto moto na za uhakika kutoka kwenye channel hii ya habari inayokuletea habari za uhakika kila siku.

From Opera News


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad