Mtayarishaji wa muziki, Master Jay, amemuomba radhi msanii wa Bongo Fleva, Alikiba, kufuatia kauli alizotoa kwenye mahojiano yake na @SimulizinaSauti.
Kupitia mahojiano na Crown FM, Master Jay amesema kuwa hana chuki wala dhamira ya kumkebehi mtu yeyote, huku akikiri kuwa maneno aliyoyasema awali hayakuwa sahihi.
“Hii ya juzi ilikuja nilikuwa nimeonja vitu kidogo na niseme tu mbele yenu, naomba Alikiba anisamehe, nilikosea,” alisema Master Jay.
Wengi wanatarajia kusikia majibu ya Alikiba kuhusu ombi hili la msamaha.