Mwenyekiti Mstaafu wa Chadema Freeman Mbowe ameendelea kuwa kimya katika maeneo yote hadi kwenye mitandao yake ya kijamii ambapo hajaweka maudhui mapya tangu aliposhindwa kwenye uchaguzi mwezi Januari mwaka huu
Kinyume na ilivyozoeleka kwa mwanasiasa huyu na mwanamageuzi mkubwa Tanzania hajaweka Post yoyote iwe kwenye mtandao wake wa Instagram au X zamani Twitter
Mbowe alizoeleka kwa kuweka post mbalimbali za masuala ya harakati na mambo yanayoendelea ndani ya chama hicho kama kampeni mpya zinazoendeshwa na chama lakini kwa wakati huu imekuwa kinyume na matarajio ya wengi mitandaoni
Ukipita kwenye mtandao wake wa X utagundua kuwa chapisho la mwisho la Mbowe ni la Januari 23 na 22 wakati akitangaza kuyapokea matokeo ya kushindwa kwake na tangia happ sasa hakuna tena andiko lolote aliloweka
Sasa ajabu ni kwamba kwenye ukurasa wake wa instagram machapusho yake ya mwisho ni Septemba 20 na 21 mwaka 2024 wakati akitangaza na kufanya maandamano ya amani mkoani Dar es salaam. Hii ina maana kuwa hata wakati wa kampeni zake hakutumia mtandao huo kujinadi licha ya uchaguzi ule kuwa wa kusisimua na wenye mvuto mkubwa.
Ukimya huu wa Mbowe unaendelea kuwaacha watu kwenye maswali wakati ambao chama chake kipo kwenye kampeni kubwa ya kuukataa uchaguzi kutokana na sheria mbovu wanazotaka zinmbadilishwe ila yeye kama Mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu hajasema chochote hadi sasa
Hivi karibuni Mbowe alionekana hadharani kwa mara ya kwanza akishiriki ibada ya mazishi ya mkwe wa waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba japo pia Mbowe hakupata nafasi ya kuzungumza na wanahabari kuhusu Ukimya wake kwa sasa
From Opera News/MsakaHabariMedia