Ndiyo maana Kocha mpya wa Harambee starz Ben Mccarthy kamjumuisha kwenye kikosi hicho
Ameandika @officialevodiusoscar_
DUKE OOGA ABUYA(30)🇰🇪 ni moja kati ya wachezaji ambao wakati Young Africans wanakamilisha uhamisho wao niliandika hapa kuwa ni moja ya maingizo bora sana ndani ya kikosi chao, kuanzia klabu aliyotoka alikuwa akicheza kikosi cha kwanza kisha muendelezo wake ulikuwa juu sana na uwezo wa kucheza maeneo mengi uwanjani unapatikana kwake
Ni mchezaji ambaye anaweza kucheza kama kiungo chini au juu lakini pia ukitaka acheze pembeni atakupa nguvu ile ile, ndani ya kikosi chako ukiwa na wachezaji wa aina hii ni faida kubwa sana, leo Mudathir Yahya hayupo ila Duke Abuya anacheza vizuri tu nafasi yake, hata Khalid Aucho na Maxi Nzengeli wakikosekana bado anaweza kucheza vizuri tu
YOUNG AFRICANS hapa walifanya moja kati ya saini bora sana katika dirisha kubwa la usajili lililopita, miguu na ubongo wake ipo haraka sana kufanya maamuzi, binafsi huwa nafurahia sana kumtazama Duke Abuya! Top Talent, One of the best signings for yellow and green Nation 🫡
Let's Goo!!.