Mchezaji wa Yanga SC, Ibrahim Hamad #IbraBacca, amepewa heshima kubwa baada ya Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo (KMKM) #Zanzibar kumpandisha cheo kutoka Koplo hadi Sajenti.
Taarifa hii imetangazwa rasmi na klabu ya #Yanga, wakimpongeza Bacca kwa juhudi na mchango wake uwanjani. Kupandishwa cheo kunathibitisha sio tu uwezo wake katika soka, bali pia nidhamu na bidii alizoonyesha kama mwanajeshi wa KMKM.
Mashabiki wa Yanga na wapenzi wa soka wameendelea kumpongeza kwa mafanikio haya, wakiamini kuwa hatua hii itampa motisha zaidi kuendelea kung’aa ndani ya kikosi cha Wananchi.