Web

Mchungaji Mashimo Ahukumiwa Miaka Miwili Jela, Kisa.....


Mchungaji Mashimo Ahukumiwa Miaka Miwili Jela, Kisa.....


Mchungaji Daud Nkuba maarufu kama Komando Mashimo amehukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani baada ya kutiwa hatiani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kwa makosa mawili ikiwemo kuharibu mali.

Mashimo alikabiliwa na mashitaka matatu ambapo Upande wa Jamhuri umethibitisha makosa mawili na kushindwa kuthibitisha shtaka la kutishia kwa vurugu kama walivyomshitaki.

Mashimo alipewa adhabu hiyo , mahakamani hapo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ramadhan Rugemalila, baada ya upande wa Jamhuri kuthibitisha makosa dhidi ya mshitakiwa pasi na kuacha shaka yoyote.

Katika hukumu hiyo, Hakimu Rugemalira alisema anamhukumu mshitakiwa kifungo cha miaka miwili gerezani kama alivyoshitakiwa na upande wa Jamhuri.

“Mshitakiwa kosa la kuingia kwa jinai mahakama inakupa adhabu ya kwenda jela miezi sita, kosa la kuharibu mali mahakama inakutia hatiani na kukupa tisa adhabu ya kwenda jela miaka miwili pia mahakama inakuachia huru kwa kosa la kutishia kwa vurugu kwasababu upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha shtaka dhidi yako , hivyo utatumikia kifungo cha miaka miwili gerezani “ alisema hakimu

Alisema upande wa Jamhuri umethibitisha kwa kuleta mashahidi watano na vielelezo pia mshitakiwa kutoa utetezi wake kwa kuleta mashahidi kadhaa.

Kabla ya kutolewa hukumu hiyo, mshitakiwa aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwasababu anafamilia inayomtegemea.

Upande wa Jamhuri wakili wa serikali Rhoda Kamungu aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa Mshitakiwa kama sheria inavyoelekeza, ikawae fundisho kwake na jamii nzima

November 22 mwaka 2023, maeneo ya Mbezi Luis Wilaya ya Ubungo Dar es Salaam, aliingia kwa jinai katika ardhi inayomilikiwa na Frola Mwashaa.

Pia mshitakiwa katika kipindi hicho kwa makusudi na kinyume cha sheria aliharibu ujenzi wa nyumba iliyoko maeneo ya Mbezi Luis ambayo ni mali ya Frola Mwashaa.

Katika shtaka la tatu ,inadaiwa alimtishia Ramson Vicent kwa vurugu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad