Rais na mfadhili wa klabu ya Simba Mohamed Dewji kwa mujibu wa Jarida la Forbes limetoa orodha ya matajiri 20 barani Afrika kwa mwaka 2025 ambapo ni matajiri wawili pekee kutoka Afrika Mashariki ambao wamepenya kwenye orodha hiyo ambao ni Mohamed Dewji mwenye Dola bilioni 1.5 za Kimarekani akiwa ameshika nafasi ya 14.
Mwingine ni Youssef Dewji akiwa na utajiri wa Dola milioni 900 za Kimarekani akiwa nafasi ya 19. Hii inakuonesha. Kwa miaka zaidi ya 10 Dewji amekua kwenye orosha ambayo imekua ikitolewa na Forbes kama ni moja ya matajiri wakubwa barani Afrika. Kwa Tanzania amekua akishikilia rekodi ya kua tajiri namba moja.
Utajiri wake ni kutokana na uwekezaji ambao ameufanya katika maeneo mbalimbali. Kumekua na ushindani na ubishani mkubwa katika mitandoa ya kijamii juu ya utajiri wa GSM ambaye ni mfadhili wa klabu ya Yanga. Wapo ambao wamekua wakieleza kua utajiri wa GSM ni zaidi ya utajiri wa Mohamed Dewji.
Kwa hiki ambacho kimeandikwa na Jarida la Forbes linadhihirisha kuwa Mohamed Dewji mfadhili wa klabu ya Simba ndiye mwenye utajiri mkubwa kuzidi mfadhili wa klabu ya Yanga Ghalib Said Mohamed (GSM). Uwekezaji ambao umefanywa katika vilabu vya Simba na Yanga umeendelea kufanya watu hawa kuzungumzwa kwa kiasi kikubwa katika vyombo vya habari.
Chanzo: The Citizen