Web

Mrembo Nicole Atuhumiwa Kutapeli Mamilioni ya Pesa Kwa Michezo wa Upatu, Akamatwa na Polisi



Mrembo Nicole Atuhumiwa Kutapeli Mamilioni ya Pesa Kwa Michezo wa Upatu, Akamatwa na Polisi



Zaidi ya Wananchi 20 kutoka Maeneo tofauti wamefika kituo cha Polisi Osterbay Masaki Jijini Dar es Salaam, wamedai kutapeliwa fedha zao na Muigizaji maarufu Nchini Tanzania, Nicole Joyberry baada ya kuanzisha mchezo wa upatu mtandaoni.


Wakizungumza na Manara TV, baada ya kufika katika eneo hilo Wananchi hao wameeleza kuwa Muigizaji huyo alitumia mitandao yake ya kijamii ikiwemo Instagram kushawishi watu kujiunga na Mchezo huo wa upatu na walishawishika kujiunga na mchezo huo kutokana na umaarufu aliokuwa nao Nicole.



Wamesema kuwa wamekuwa wakichez mchezo huo bila ya kuwepo na mafanikio yoyote na walipotaka kuhoji juu ya hatma ya fedha zao Muigizaji huyo hakutaka kuonyesha ushirikiano wa aina yoyote.

Aidha wamesema kuwa Tayari Muiguzaji huyo yuko mikononi mwa Jeshi la Polisi kwaajili ya Uchunguzi zaidi.

Akizungumza mmoja wa waanga aliyejitambulisha kwa jina la Jonsoni alisema kuwa alitapeliwa milioni 7, ambapo raundi ya kwanza walicheza akawalipa lakini mzunguko wa pili aanza kuzungusha watu.



Aliongeza kuwa baada ya kufatilia aligundua kuwa amewatapeli watu wengi sana kwenye magroup na baada ya kufatilia walitoa taarifa kwenye kwa jeshi la polisi.

Naye Marian alisema kuwa yeye ametapeliwa milioni 14 ambapo amesema kuwa alikuwa anacheza elfu sabini na kwa wiki alikuwa anacheza laki tatu.

Chanzo Manara Tv

From Opera News

Maudhui yaliyoundwa na kutolewa na MatukioHabari . Opera News ni jukwaa huru hivyo maono na maoni yaliyotolewa humu ni ya mwandishi pekee na hayawakilishi, hayaakisi au hayatoi maoni ya Opera News. Maudhui yoyote/yote yaliyoandikwa na picha zinazoonyeshwa hutolewa na mwanablogu/mwandishi, huonekana humu kama ilivyowasilishwa na mwanablogu/mwandishi na hazijahaririwa na Opera News. Opera News haikubaliani na uchapishaji wa maudhui yoyote ambayo yanakiuka haki (ikiwa ni pamoja na hakimiliki) za wahusika wengine, wala maudhui ambayo yanaweza kuchafua, pamoja na mengine, dini yoyote, kabila, shirika, jinsia, kampuni, au mtu binafsi. Habari za Opera pia haziungi mkono matumizi ya jukwaa letu kwa madhumuni ya kuhimiza/kuidhinisha matamshi ya chuki, ukiukaji wa haki za binadamu na/au matamshi ya asili ya kukashifu. Iwapo maudhui yaliyomo humu yanakiuka haki zako zozote, ikiwa ni pamoja na zile za hakimiliki, na/au kukiuka vipengele vyovyote vilivyotajwa hapo juu, unaombwa kutuarifu mara moja ukitumia barua pepe ifuatayo feedback-opera-news-app@opera.com na/au ripoti makala kwa kutumia sehemu ya kuripoti iliyojumuishwa katika Mfumo wetu.Read more>>l

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad