Klabu ya Simba Sc kupitia kwa mwenyekiti wa wanachama wa klabu hiyo mzee Murtaza Mangungu wameoa msimamo wao mgumu juu ya hatma ya sakata la kuahirishwa kwa dabi ya kariakoo ikiwa ni pamoja na majibu kwa watania wao wa jadi Yanga Sc.
Murtaza Mangungu katika taarifa yake aliyoitoa siku ya jana Jumamosi tarehe 22 Machi, kupitia "Mpenjatv" alitoa fumbo zito ambalo lilikuwa linaeleza kwamba "usidai haki kama hautendi haki, ili upate haki tenda haki".
Taarifa hii fupi kutoka kwa Mangungu imetafsiriwa kwamba Mangungu amelenga kuwajibu Yanga Sc ambao mpaka sasa wanashinikiza kudai haki yao kwa bodi ya ligi na hapa wanahitaji kupewa alama tatu za mezani kwa sababu wanaamini kwamba Simba Sc walifanya kosa la makusudi kwa kugomea mechi ya dabi ya kariakoo.
Yanga Sc katika maandiko na vikao kadhaa wanavyoendelea kuvifanya hivi karibuni kupitia kwa wanachama wao wameonyesha wazi kwamba wanadai yaki yao ya kupata alama tatu kwenye bodi ya ligi na hawataki kucheza mchezo mwingine dhidi ya Simba Sc.
Mangungu katika taarifa yake amelenga kuwakumbusha Yanga Sc kwamba hawana sababu ya kudai haki hii kwa sababu wao hawakutenda haki kwa Simba Sc kwani waliwanyima haki yao ya msingi ya kufanya mazoezi ya mwisho siku moja kabla ya mchezo wa dabi ya kariakoo.
Murtaza Mangungu pia amegusia msimamo wa klabu hiyo kuhusiana na tukio hilo ambapo ameeleza wazi kwamba wao kama Simba Sc kwa sasa hawawezi kusema jambo lolote mpaka pale bodi ya ligi itakapo toa maamuzi yake kwa sababu suala hili kwa sasa liko chini ya uchunguzi wa mamlaka hiyo.
Katika hili Simba Sc wamechagua kuwa tofauti na Yanga Sc ambao kwa hivi karibuni wameonyesha kufanya baadhi ya mambo ambayo yanawashinikiza viongozi wa bodi ya ligi kufanya maamuzi haraka kitu ambacho ni nje na utaratibu wao kama bodi.
Simba Sc katika sakata hili wamejiweka pembeni sana kwa sababu wanaamini kwamba wao ndio wenye hali zaidi ya Yanga Sc kutokana na tukio walilokuwa wamefanyiwa siku moja kabla ya mchezo na watu wanaodaiwa kuwa ni wanachama wa klabu ya Yanga Sc.
Simba Sc na Yanga Sc kwa sasa wote wanabaki kuwa chini ya sheria na wanasubiri majibu na maamuzi kutoka bodi ya ligi ambao ndio mabosi au waendeshaji wakuu wa mpira wa miguu nchini Tanzania.
From Opera News
Sports_HQ