Web

Mwamba Jela Maisha Kwa Kumlawiti Mtoto wa Miaka Minne

Mwamba Jela Maisha Kwa Kumlawiti Mtoto wa Miaka Minne


MAHAKAMA ya Wilaya ya Iramba Mkoani Singida imemhukumu kifungo cha maisha jela Barnaba Yohana Isaya (20), mkazi wa kiji cha Nselembwe, kata ya Sherui, Wilayani humo kwa kosa la kumlawiti mtoto wa kiume miaka minne (4) Mkazi wa kiji hicho.


Mara baada ya kutenda kosa hilo, Mtuhumiwa alikamatwa na Jeshi la Polisi Februari 5, 2024 katika kijiji cha Nselembwe, ambapo alifikishwa Mahakamani Februari 12, 2025 kujibu tuhuma zinazomkabili.


Akitoa hukumu hiyo Machi 6, 2025 hakimu wa Mahakama hiyo, Mhe. Simon Kayinga ameeleza kuwa baada ya Mahakama kujiridhisha pasi na shaka na maelezo ya mashahidi, mshitakiwa ametiwa hatiani na atatumikia kifungo cha maisha jela kwa kosa hilo la ukatili.


Mheshimiwa Kayinga amesema adhabu hiyo ikawe fundisho kwa watu wenye tabia za ukatili kama huo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad