Web

Mzee Atapeliwa Akitaka Utajiri Kwa Mganga, Aachwa Makaburini Akiwa Uchi




Mzee Mussa Rashid ambaye ni Mkazi wa Tabora, ametapeliwa pesa Tsh. laki mbili, simu, kadi ya CCM na kadi ya NIDA, suti yake ya gharama kubwa na saa yake yenye thamani ya Tsh. milioni moja baada ya kusafiri hadi Sumbawanga Mkoani Rukwa akiufuata utajiri wa haraka kwa Mganga wa kienyeji ambaye ameishia kumtapeli na kumkimbia.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana March 14,2025, ambapo Mzee huyo (anayeonekana kwenye picha) aliwasili Sumbawanga March 13,2025 saa 4 usiku na kukutana na Mwenyeji wake, ambaye alimtaka aoge dawa maalum kabla ya tiba kuendelea kisha baada ya muda mfupi, alipelekwa makaburini ambapo alilazwa juu ya kaburi na kuanza kuogeshwa dawa akiwa uchi wa mnyama kabla ya kutapeliwa na akatelekezwa hapo akiwa utupu hadi Wasamaria wema walipomuokota na kumstiri kwa kipande cha kanga.

Mzee huyo amesema “Nilipokutana na Mganga akaniambia chukua maji ya Tsh.500 nikachukua madogo mawili, tukaenda hadi makaburini, akaniambia chukua madongo ardhini tumefika akapaka lile kaburi yale madongo, akaniambia lala juu ya kaburi wakati huo nimeshavua nguo zote, akanimwagia dawa zake, akaniambia nenda pale ulipochukua mchanga na madongo nenda kaombe unachotaka pale, nikaenda kurudi sijamkuta, laki mbili imechukuliwa, simu imechukuliwa, saa ya gharama ya milioni moja imechukuliwa, kadi ya CCM na kadi ya NIDA vyote vimechukuliwa, suti yangu imechukuliwa”

Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Nyakia Ally Chirukile amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amewataka Watanzania kuachana na imani potofu za kutafuta utajiri kwa njia za kishirikina huku akihimiza Wananchi kufanya kazi kwa bidii na kumtanguliza Mwenyezi Mungu badala ya kutegemea Waganga wa kienyeji wasiokuwa na uaminifu na kuwataka Watu waache kujidanganya kuwa Sumbawanga kuna utajiri… Polisi tayari wameanza kumtafuta Mganga huyo feki.

Source: Millard Ayo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad