Web

Nafasi za Kazi Jeshi la Polisi Zatangazwa Leo


Nafasi za Kazi Jeshi la Polisi Zatangazwa Leo

Nafasi za Kazi Jeshi la Polisi Zatangazwa Leo 

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi limetangaza nafasi za ajira kwa vijana wa Kitanzania wenye elimu ya shahada, stashahada, astashahada, kidato cha sita na cha nne wenye sifa mbalimbali.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Camilius Wambura, Machi 20, 2025 vijana wanaohitajika wanatakiwa kuwa raia wa Tanzania kwa kuzaliwa, wazazi wawe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa na awe amehitimu kidato cha nne au cha sita kuanzia mwaka 2019 hadi 2024.

Sifa nyingine ni waombaji wa kidato cha nne, cha sita na wenye astashahada awe na umri kuanzia miaka 18 hadi 25, kwa waombaji wa kidato cha nne wawe na ufaulu wa daraja la kwanza mpaka la nne.

Kwa waombaji wenye ufaulu wa daraja la nne wawe na ufaulu wa alama 26 hadi 28, huku waombaji wa kidato cha sita wawe na ufaulu wa daraja la kwanza hadi la tatu. Wahitimu wa shahada na stashahada wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi 30, urefu usiopungua futi tano na inchi nane (5’8”) kwa wanaume na futi tano inchi nne (5’4”) kwa wanawake.

Sifa nyingine ni kuwa na kitambulisho cha Taifa au namba ya utambulisho kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), uwezo wa kuongea Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha na afya njema kimwili na kiakili iliyothibitishwa na daktari wa Serikali.

Muombaji anatakiwa kuwa hajaoa, kuolewa au kuwa na mtoto ama watoto, hajawahi kutumia dawa za kulevya za aina yoyote, kuwa tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya taaluma ya Polisi na awe hajaajiriwa au hajawahi kuajiriwa na taasisi nyingine ya Serikali.

Anatakiwa kuwa tayari kufanya kazi za Polisi mahali popote Tanzania, kujigharimia katika hatua zote za usaili endapo ataitwa kwenye usaili, asiwe na alama za kuchorwa mwilini (tattoo) wala kumbukumbu za uhalifu.

Kwa waombaji wenye elimu ya kiwango cha shahada (NTA level 8), stashahada (NTA level 6) na astashahada (NTA Level 5 au NVA Level 3) wanatakiwa kuwa na fani zilizoainishwa kwenye tangazo la nafasi za ajira.

Waombaji wote wanatakiwa waandike barua za maombi wao wenyewe kwa mkono bila kusahau namba za simu na watumie anuani ya Mkuu wa Jeshi la Polisi S.L.P 961 Dodoma. Barua hiyo iambatishwe kwenye maombi ikiwa kwenye mfumo wa ‘pdf’.

JISNI YA KUAPPLY NAFASI ZA POLISI 

Waombaji wote wanatakiwa wafanye maombi kupitia kwenye mfumo wa Ajira wa Polisi (Tanzania Police Force – Recruitment Portal) unaopatikana kwenye kiunganishi (link) cha tovuti ya Jeshi la Polisi (https://ajira.tpf.go.tz).

“Maombi yatakayowasilishwa kwa njia ya posta, barua pepe (email) au kwa mkono hayatapokelewa,” limeeleza tangazo hilo.

Mwisho wa kupokea maombi ni Aprili 4, 2025.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad