Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania maarufu kama Taifa Stars Hemed Morroco asubuhi ya Ijumaa ya tarehe 14 mwezi wa 03 mwaka 2025 ametoa orodha ya majina ya wachezaji ambao wataingia kambini kwa ajili ya kuiwakilisha timu ya taifa ya Tanzania kwenye mchezo dhidi ya taifa la Morocco kwa ajili kuwania nafasi ya kufuzu kucheza kombe la dunia mwaka 2026 ambalo litachezewa nchini Marekani.
Kocha Hemed Morroco ambaye amefanikiwa tayari kuisaidia timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kufuzu kucheza michuano ijayo ya kombe la mataifa ya Afrika AFCON kwa sasa yupo kwenye hatua za kuijenga timu ya taifa ya Tanzania ili kuwa na timu imara ya taifa ambayo itaweza kupambana kufuzu kucheza kombe la dunia mwaka 2026.
Wachezaji ambao wameitwa kwenye timu ya taifa ya Tanzania wengi wametoka kwenye timu za Simba Sc pamoja na timu ya Yanga Sc huku mlinzi wa kulia wa timu ya Simba Sc akirejea kwenye timu ya taifa ya Tanzania tena baada ya kuachwa mara kwa mara kwenye timu hiyo, huku mshambuliaji wa timu ya taifa na nahodha Mbwana Samatta akiwa ameachwa nje ya kikosi kwa sababu ya majeruhi.