Msanii na mfanyabiashara Sean "Diddy" Combs, akiwa gerezani, alimfanya #KanyeWest (Ye) kuwa mmoja wa watu wachache wa kuaminika kwake. Katika mazungumzo yaliyovuja, #Diddy alimpa Ye ushauri wa kurudi kwenye ubunifu na kufurahia muziki, akidai kuwa mambo yamekuwa "mabaya mno" kwenye tasnia.
"Nataka kukuona ukirudi jukwaani, ukiimba tena, ukiwasha moto," alisema Diddy kwa msisitizo. "Usiwajali hao watu wengine, wana kupotezea muda."
Kanye alimjibu kwa kusema kuwa ameanza "kuupenda muziki tena" baada ya kipindi kigumu. Diddy alihimiza kuwa bado kuna muda wa kupigania haki, lakini ni muhimu kwa Ye kufurahia maisha.
Katika mazungumzo hayo, Diddy pia alimshukuru Kanye kwa kuwa mmoja wa watu wachache waliobaki upande wake huku wengine waliomsapoti hapo mwanzo wakimgeuka. Sehemu ya simu hiyo ilihusishwa na wimbo wa Kanye uliovuja, "Lonely Roads Still Go to Sunshine," ambao unamshirikisha Diddy, #NorthWest, #KingCombs, na msanii mpya wa Yeezy kutoka Chicago, #JasmineWilliams.
Aidha, mazungumzo yao yaliangazia mgogoro wa Kanye na aliyekuwa mke wake, #KimKardashian, kuhusu haki za jina la binti yao, North West. Kanye alitaka North aonekane kwenye wimbo huo, lakini Kim alipingana naye na kufikiria hatua za kisheria dhidi yake.
Mazungumzo haya yamezua mijadala mikali mtandaoni, huku wengi wakishangazwa na ukaribu wa wawili hao katika kipindi ambacho Diddy anakabiliwa na kesi nzito.
SNS