Web

Phina Awatuliza Mashabiki Baada ya Kuikataa Colabo na Willy Paul wa Kenya



Baada ya mashabiki wa Tanzania kuonyesha kutokukubaliana na ushirikiano kati ya Phina na Willy Paul, msanii huyo wa Bongo Fleva ameandika ujumbe wa kuwatuliza na kuwakumbusha kuwa muziki hauna mipaka.

Mashabiki wengi wa Tanzania wamekuwa wakimkosoa #WillyPaul kutokana na kauli zake za zamani, ambazo zilionekana kudharau wasanii wa Bongo Fleva. Kutokana na historia hiyo, baadhi yao wamepinga waziwazi ushirikiano wake na Phina, wakihisi kuwa hana heshima kwa wasanii wa Tanzania.

Hata hivyo, Phina amewataka mashabiki kutokupoteza "FOCUS", akisisitiza kuwa jambo muhimu ni muziki na sio migogoro ya zamani. Ameeleza kuwa yeye si sehemu ya "timu" za ushindani bali anasimamia muziki kama daraja la kuunganisha Afrika Mashariki.

Kwenye ujumbe wake, Phina amesisitiza upendo kwa mashabiki wake wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, akihimiza mshikamano na kuacha tofauti za kikanda ziwe kikwazo kwa wasanii kushirikiana.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad