Msemaji maarufu wa mpira kupitia klabu ya mpira wa miguu Yanga Sc ambayo inaongoza ligi hapa nchini Tanzania almaarufu kama Ali Kamwe. Siku ya leo azua gumzo kwenye vyombo vya habari baada ya taarifa yake hii kusambaa kwenye vyombo vya habari hasa Instagram.
Licha ya kwamba soka la bongo kuna wachezaji wengi wazuri wa ndani na nje ya nchi ambao kwa namna moja ama nyingine wamechangia kukua kwa soko letu Afrika, lakini pia uwepo wa wasemaji mahari wa timu hasa Simba na Yanga umeongeza mvuto mkubwa katika soka. Wapo waandishi kadhaa ambao nyuma walipita mfano Haji Sunday Manara pia walifanya vizuri sana, mpaka Ally Kamwe na Ahmed Ally kuchukua umaarufu huo miaka ya hivi karibuni.
Licha ya watu hawa kuwa huru kusemea timu zao popote wanapoenda ili wasionekane wanyonge pamoja na kuhamasisha mashabiki zao, lakini watu hawa wanazungukwa na sheria kali kutoka kwenye taasisi ambayo inasimamia maswala yote ya soka hapa nchini yaani TFF. Takribani mwezi mmoja umepita tangu TFF ilipowatia hatiani wasemaji wa mpira wa miguu hapa nchini yaani msemaji wa Yanga, Simba na Tabora United.
Wasemaji hawa walituhumiwa kwa kosa la kutoa kauli chafu ambazo zinaharibu taswira ya mpira wa bongo. Sasa siku ya leo inasemekana kuwa wasemaji hao waliitwa kwenye kikao cha nidhamu cha TFF ili kujibu kesi zao. Hata hivyo inasemekana kuwa Ali Kamwe amefungiwa miaka miwili kufanya kazi hiyo na hatakiwi kabisa kujihusisha na mpira. Lakini pia katika hukumu hiyo inasemekana pia Ahmed Ally hana hatia na anaendelea na majukumu yake kama kawaida.
Taarifa hizi ni taarifa za awali za kesi hiyo huku zikisema kwamba baada ya mchezo wa Simba na Yanga tarehe 08 mwezi huu, basi TFF watatoa taarifa rasmi kuhusiana na kesi hiyo. Taarifa hii imewashtua sana wapenzi wa soka nchini hasa kwa upande wa klabu ya Yanga, huku mashabiki wa Simba wakibaki na furaha.
Wasemaji wa mpira wanaweza fanya soka likawa vizuri endapo wakatumia vizuri nafasi zao, lakini pia wanaweza haribu mpira endapo wakatumia vibaya taaluma zao. Kwa upande wa waandishi wetu walikuwa wanavuka sana mipaka ya kazi yao, hivyo kukosekana kwa utulivu kwenye mpira.
Mpenzi msomaji wa habari hii, unalipi la kusema kuhusiana na taarifa hii ? Tafadhali weka maoni yako chini ya habari hii pia usisahau kulike, kushare na kufollow ukurasa huu ili uwe mtu wa kwanza kupata habari zangu pindi zinapotoka.
Chanzo: David Pascol
From Opera News