Web

Polisi Mkoani Geita Wakamata Mzigo wa Dhahabu Wenye Thamani ya Milioni 700

Top Post Ad

Polisi Mkoani Geita Wakamata Mzigo wa Dhahabu Wenye Thamani ya Milioni 700


Polisi Mkoani Geita linawashikilia watu watatu waliokutwa na gramu 3,263.72 za dhahabu yenye thamani ya shilingi 749,509,531.94 ambazo walikuwa wakizisafirisha kwa njia za magendo kwa kutumia gari aina ya Toyota Premio yenye namba za usajili T.739 EEH mali ya Emanuel Kidenya Mkazi wa Kahama, Shinyanga.

Waliokamatwa ni Yohana Idama (34), Mkazi ya Nyamhongolo wilaya ya Ilemela Mwanza, Moshi Manzili (26), Mkazi wa Bariadi Simiyu na Hamidu Salum (25), Mkazi wa Nyasubi wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Watuhumiwa hao wamekamatwa Machi 24, 2025 majira ya saa 5 usiku katika Mtaa wa Kapera Wilayani Bukombe baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa za siri na kuweka mtego uliofanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao.

Uchunguzi wa tukio hili kwa kushirikiana na Mamlaka nyingine unaendelea kufanyika sambamba na kubaini na kuwakamata watakaobainika kujihusisha na uhalifu huo na kuwafikisha Mahakamani mara moja.

Jeshi la Polisi katika taarifa yake kupitia kwa Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Geita, limetoa wito kwa wananchi kuacha mara moja kujihusisha na vitendo vya magendo na biashara haramu kwani halitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo.

Below Post Ad

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.