Waziri wa zamani wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Profesa Philemon Sarungi amefariki dunia March 05,2025 saa kumi jioni Jijini Dar es salaam.
Taarifa iliyotolewa na Martin Leonard Obwago Sarungi, Msemaji wa Familia ya Chifu Sarungi imeeleza yafuatayo “Familia ya Chifu Sarungi na ukoo wa Nyiratho wa Utegi, Rorya, tunasikitika kutangaza kifo cha Mpendwa wetu Mzee Professor Philemon Mikol Sarungi kilichotokea leo tarehe 05/03/2025 saa kumi jioni, msiba upo nyumbani Oysterbay Mtaa wa Msasani Dar es salaam”
“Taarifa na taratibu nyingine zitatolewa na Familia, apumzike kwa amani Mzee wetu”