Web

Rais Kapteni Ibrahim Traoré Amfukuza Kazi Waziri Aliyepanga Njama za Kumuua




Kapteni Ibrahim Traoré, ambaye anaongoza utawala wa kijeshi nchini Burkina Faso, ameamua kujitenga na Waziri Mkuu wake na kuondoa baadhi ya watu ambao hana imani nao katika serikali yake kutokana na mfululizo wa matukio ya majaribio ya kifo.



Apollinaire Kyelem de Tambèla ambaye alikuwa Waziri Mkuu mara mbili mfululizo amefukuzwa katika nafasi hiyo kutokana na kile kinacho daiwa msaliti kwa kula njama ya kutaka Kumuua Ibrahim Traore katika Jaribio la sumu ambayo aliwekewe kwenye chakula Ikulu.

Katika taarifa za ndani zilisema kuwa licha ya Jaribio la kwanza la kumwekea sumu kwenye chakula Waziri alishiri njama nyingine katika shambulio la Mita 2 Kutoka Kifo.

Cha ajabu, Licha ya kumtumbua Ibrahim Traore hakutaka kuweka wazi sababu iliyo mfanya amtumbue Kwa sababu endapo angesema kuwa Waziri Mkuu amehusika katika Jaribio la Kumuua Traore basi Raia wangezua taharuki na maisha ya Waziri yangekuwa hatarini jambo ambalo hakutaka litokee Kwa haraka.



Hii ni kwa sababu hukumu ya Msaliti katika Taifa hilo ni kifo Cha kunyongwa jambo ambalo Ibrahim Traore hakutaka litokee Kwa Waziri Apollinaire Kyelem de Tambèla.

Kapteni Ibrahim Traore ambaye anaongoza utawala wa kijeshi nchini Burkinafaso alisema kwamba kumuondoa madarakani Waziri huyo ni jambo la busara zaidi, kwani hafikilii kufanya kibaya dhidi yake ili kuepusha sintofahamu.

Baadhi wa Wana diplomasia waliunga mkono maamuzi ya Ibrahim Traore kwani ametumia hekima zaidi kuliko cheo. Kwa Mujibu Wa kanuni Waziri alipaswa kunyongwa mpaka kufa hadharani bila huruma. Jambo ambalo lingezua mjadala mkubwa katika mataifa ya mbali.



Lakini pia baadhi ya wadau wamelaani vikali tukio hilo la usaliti ambalo linafanywa na baadhi ya watu walio aminiwa na umma Kwa ajili ya kuitetea nchi yao kama ilivyo Kwa Waziri.

Wengine wakisema adui Yako ni ndugu wa karibu, Waziri mwenye dhamana na kuungana na Rais Leo hii anafanya usaliti Kwa ajili ya Kumuua mwenzio Kwa tamaa ya uchu wa madaraka na ushawishi kutoka nchi za mbali. Jambo ambalo halipaswi kufanyika hata mara Moja.

Lakini pia wapo wadau walio sema ni kheri angenyongwa ili kuleta fundisho Kwa viongozi wengine ambao Wana tabia za kusaliti viongozi wao walio wazidi vyeo.


Je, Traore alikuwa sahihi kumuondoka madarakani bila kumchukulia hatua Kali yeyote kama vile kufungwa jela au kuuawa?

By Mohobland_News

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad