Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa Dini wasidandie ajenda au vishawishi vya kisiasa na kuvuruga amani ambapo amesisitiza majukwaa ya Ibada yatumike kwa Ibada na yasitumike na Wanasiasa kufanyia propaganda zao.
Akiongea Jijini Dar es salaam leo March 31,2025 kwenye Baraza la Eid El Fitr, Rais Samia amesema ““Matarajio yetu ni kuwa majukwaa ya Dini yatafanya kazi ya kulinda amani pale Wanasiasa watakapotibua utulivu ndani ya nchi yetu”
“Serikali kwa upande wake tutasimamia na kuheshimu misingi ya Katiba ya kuheshimu uhuru wa Raia wa kuabudu na kuubiri Dini ila kamwe hatutomvumilia yeyoye atakayetumia haki hii kuchochea chuki na uhasama, tumeapa kulinda haki na utu wa kila Mtanzania hivyo hatutosita kufanya wajibu wetu bila uoga, Waswahili husema mchelea Mwana kulia basi hulia yeye basi nasi hatutokubali kulia sisi na tukamuacha Mwana atovuke, Mwana yeyote atakayetovuka tutashughulika nae ili kulinda wengi wasilie”