Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Masasi Bw. Lauteri John Kanoni na kumteua Bi. Rachel Stephen Kasanda kujaza nafasi yake.
Raia Samia pia kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka leo Machi 25, 2025. amemteua Prof. Jafari Kideghesho kuwa Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya mfuko wa uhifadhi wa wanyamapori Tanzania huku pia CPA Ashraph Yusuph Abdulkarim akiteuliwa kuwa Meneja Mkuu wa shirika la masoko Kariakoo.
Rais Samia pia katika mabadiliko yake kadhaa na upangaji wa vituo vya kazi kwa wateule wake, amempangia kituo cha Kazi Balozi Mobhare Matinyi ambapo ataiwakilisha Tanzania nchini Sweden.Kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi, Mobhare Matinyi alikuwa msemaji mkuu wa serikali na Mkurugenzi wa Idara ya habari-MAELEZO.