Web

Rais Samia Awateua Viongozi Watano

Rais Samia Awateua Viongozi Watano


Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Ismael Aaron Kimirei kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) kwa kipindi cha pili na amemteua pia Balozi Ernest Jumbe Mangu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa kipindi cha pili.

Rais Samia amemteua pia Dkt. Marina Alois Njelekela kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOl) akichukua nafasi ya Prof. Charles Mkony ambaye amemaliza muda wake.

Amemteua Juma Hassan Fimbo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na Prof. James Epiphan Mdoe kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR)akichukua nafasi ya Dkt. Andrew Kitua ambaye amemaliza muda wake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad