Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameondoka kwa hasira katika Ikulu ya Marekani (White House) baada ya majibizano makali na Rais wa Marekani Donald Trump na Makamu wake JD Vance.
Katika tukio hilo liliooneshwa moja kwa moja kutoka White House na vyombo vya habari vya Marekani , Rais wa Ukraine anaonekana akitoka nje ofisi na kuingia kwenye gari nyeusi aina ya SUV, ambayo iliondoka kwa kwa haraka.
Rais wa Ukraine ameondoka kwa hasira baada ya kulumbana na Trump ambapo muda mfupi baadaye, Trump ameandika kwenye mtandao wake wa Kijamii wa Truth Social akidai kwamba Zelensky ameidharau Marekani katika Ofisi yake inayopendwa na kusema anaweza kurejea akiwa tayari kwa mazungumzo ya amani.
Wakati wa mzozo huo Trump amemuambia Zelensky kwamba anacheza na vita ya tatu ya dunia baada ya Zelensky kuonekana kutounga mkono mazungumzo ya Trump na makamu wake kuhusu namna Ukraine inavyoshughulika na vita yake na Urusi ambapo kwa upande wake Zelensky amemwambia Trump ‘usimchekee muuaji’, akimlenga Rais wa Urusi, Vladmir Putin kwakuwa Marekani inataka Ukraine ikubaliane na Urusi kumaliza mzozo huo kwa namna ambayo Zelensky hakubaliano nayo.