Web

RIPOTI YA CAG: Bilioni 441+ Hasara Kwa Mashirika ya TTCL, TRC na ATCL

Top Post Ad

RIPOTI YA CAG: Bilioni 441+ Hasara Kwa Mashirika ya TTCL, TRC, ATCL


Mashirika kadhaa yalipata hasara, Shirika la Reli Tanzania (TRC) lilipata hasara ya Tsh. Bilioni 224 ikilinganishwa na hasara ya Tsh. Bilioni 102 ya Mwaka uliopita. Hasara hiyo ilichangiwa na uhaba wa Usafirishaji uliotokana na uhaba wa Vichwa vya Treni na Mvua kubwa iliyosababisha njia kufungwa kwa Miezi minne, kama ruzuku isingetolewa Shirika lingepata hasara ya Tsh. Bilioni 253

Hasara hii ni hadi Juni 30, 2024 kabla ya kuanza kutumika kwa Treni ya SGR."

"Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) lilipata hasara ya Shilingi bilioni 27.78 mwaka wa Fedha wa 2023/2024. Ongezeko hili ni kutoka Shilingi bilioni 4.32 ya hasara kwa mwaka uliopita. Hasara hii ya mwaka huu inachangiwa na ongezeko la gharama baada ya kuhamishiwa Mkongo wa Taifa na Kituo cha Taifa cha Data." -

"Kampuni ya Ndege Tanzania ilipata hasara ya Tsh. Bilioni 91.8 ikiwa ni ongezeko la 62% tofauti na ilivyokuwa Mwaka uliopita

Hasara hiyo imetokana na gharama kubwa za matengenezo ya Ndege na hitilafu za Injini ambapo Ndege za AirBus zilikaa muda mrefu bila kufanya kazi zikisubiri Injini."

Kampuni ilitumia Tsh. Bilioni 99.8 ikiwa ni Ruzuku kutoka Serikalini na kama isingetolewa hasara halisi ingefikia Tsh. Bilioni 191.6" Charles Kichere, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Below Post Ad

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.