SABABU ZA KUAHIRISHA MECHI NI 3 TU ZILIZOAINISHWA NA FIFA NA ZINATUMIKA DUNIANI KOTE 📌
Shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA linatambua kutokea Kwa dharula mbalimbali ambazo huweza kupelekea Mchezo husika kutochezwa kwa wakati pangwa,Kwahiyo waliweka taratibu za msingi zitakazotumika kuahirisha Mchezo husika.
Sababu hizo ni👇:
1. MABADILIKO YA GHAFLA YA HALI YA HEWA:
-Ikiwa masaa 3-5 kabla ya mchezo kuchezwa ikatokea hali mbaya ya mabadiliko ya hali ya hewa ambayo itaonekana kusababisha madhara kwa binadamu na miundombinu ya sehemu ambapo Mchezo utachezwa, mfano kuanguka kwa barafu jingi ,kimbunga kikali au mvua kubwa yenye kusababisha kujaa maji eneo la kuchezea.
Kutokana na hali hiyo Mchezo huo unapaswa kuahirishwa na Bodi ya ligi kuu au shirikisho la mpira wa miguu la nchi husika Kwa ajili ya kulinda afya za watu wote zaidi na eneo la kuchezea kuandaliwa upya Kisha Mchezo utapangiwa tarehe nyingine.
2. MASUALA YA KIUSALAMA:
-Ikitokea siku ya Mchezo husika kukawa na hali ya taharuki katika eneo la mchezo,mfano kukatokea machafuko ya kisiasa au mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yenye kusababisha vifo vya halaiki, Mchezo huo utalazimka kuahirishwa kwasababu ya kulinda maisha ya watu wote kuanzia wachezaji mpaka mashabiki.
Hapa inazungumziwa vurugu zenye kutumia silaha Kali,mfano bunduki,mapanga n.k na sio mizozo ya mashabiki nje ya eneo la uwanja,ambayo Polisi au jeshi linaweza izuia kwa dakika chache tu.
SABABU YA TATU HII HAPA✍️
3. KIFO:
-Ikitokea masaa 3-5 kabla ya mchezo kuanza,kukawa Kuna mtu kafariki na ni mmoja kati ya watu waliotambuliwa kuwa sehemu ya Mchezo huo,mfano daktari wa timu yoyote kati hizo mbili zinazocheza Mchezo huo au mwamuzi,ni dhahiri Mchezo huo utaahirishwa na kupangiwa tarehe nyingine mara moja.
*Pili ikitokea shabiki akafariki Dunia ndani ya muda wa mechi ikiwa inachezwa Mchezo huo utasitishwa mara moja na kupangiwa tarehe nyingine ya kuja kuendelea pale ulipoishia.
*Tatu ni kifo Cha kiongozi mkubwa wa nchi husika,mfano Raisi, mfalme au waziri mkuu wa taifa husika atafariki,michezo yote itaahirishwa mara moja kwa mujibu wa kanuni kupisha shughuli zitakazosimamiwa na Serikali kumuenzi kiongozi huyo,hakuna mechi itachezwa kama Kuna kiongozi mkubwa atafikwa na mauti✅.
Hakuna kifungu Cha kuahirisha mechi kwasababu timu imegoma kushiriki mchezo husika.
Timu yoyote ikigoma kuingia uwanjani mwamuzi kapewa miongozo maalumu ya kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa ikiwa ni kuingiza timu uwanjani ambayo imeridhia kucheza mchezo husika kish kusubiri dakika 15’ timu iliyogoma ifike uwanjani na isipofika mwamuzi kapewa dhamana ya kuipa point 3 na mabao 3 timu iliyokubali kufika uwanjani.
Bodi ya ligi ya taifa lolote hauruhusiwi kuahirisha mechi nje ya sababu zote hizo ni kosa kisheria.