Serikali ya Uingereza imetangaza kuipa mkopo nchi ya Ukraine wa kiasi cha Paundi bilioni 2.26 kwa ajili ya kununua silaha za kijeshi ili izidi kujiimarisha na kujilinda dhidi ya Urusi.
Makubaliano ya mkopo huo yamefikiwa baada ya Waziri Mkuu wa Uingereza Sir Keir Starmer kukutana na Volodymyr Zelensky Jijini London ambapo Sir Starmer amemwambia Zelensky kuwa anaungwa mkono kikamilifu kote Uingereza.
Zelensky na Sir Keir pia wametia saini mkopo huo kwa ajili ya vifaa vya kijeshi vya Ukraine, ambao utalipwa kwa kutumia faida kutoka kwenye mali ya Urusi iliyohifadhiwa nchini Ukraine.
Waziri Mkuu huyo wa Uingereza atakuwa Mwenyeji wa mkutano wa kilele wa Viongozi wa Ulaya Jijini London leo Jumapili kuhusu juhudi za kumaliza vita vya Urusi na Ukraine, pamoja na ulinzi mpana wa Ulaya, huku Zelensky pia akitarajiwa kukutana na Mfalme Charles III.
Itakumbukwa Marekani chini ya utawala wa Rais Donald Trump imetangaza kuwa haitoendelea tena kuisaidia Ukraine kifedha wala silaha za kivita kwasababu kipaumbele cha Marekani ni majadiliano ya amani na kumaliza vita ya Ukraine na Urusi ambapo uamuzi huu wa Marekani umetangazwa usiku wa kuamkia jana March 01,2025 na Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Caroline Leavitt baada ya kupira siku moja tangu Trump na Rais wa Ukraine Zelensky wazozane mbele ya camera za Waandishi wa Habari.