Web

Shaffih Dauda: Yafanyike Mageuzi Mpira Uongozwe na Wenye Sifa Uongozi wa Soka

Shaffih Dauda: Yafanyike Mageuzi Mpira Uongozwe na Wenye Sifa Uongozi wa Soka


Tanzania ina bahati ya kuwa na Ligi yenye ushindani na yenye mvuto wa kibiashara, kama hakuna mtu wa kusafisha hali ya sasa, mediocrity itaendelea kutawala.

Suluhisho linapaswa kuwa

• FIFA ichukue hatua kali kwa TPLB na mamlaka za soka nchini ( Wote wanaosimamia mpira)

• Yafanyike Mageuzi ya utawala wa soka na kuhakikisha viongozi wanakuwa na sifa rasmi za kiutawala hasa wa mpira ( Mpira uongozwe na watu wa mpira) Hii ni kuanzia Ngazi za Juu , Vilabu hadi chini kabisa.

• Vyombo vya habari virudi kwenye msingi wa kuhabarisha , kuelimisha , kukosoa, kuburudisha inapobidi na uchambuzi wa kweli badala ya ushabiki

• Mashabiki waache ushabiki wa kipofu na waweke shinikizo kwa mamlaka za soka kuboresha hali ya ligi

Kwa sasa, Tanzania imefika mahali ambapo mediocrity imehalalishwa—mashabiki, viongozi, vyombo vya habari, na hata baadhi ya wachezaji wanaishi ndani ya mfumo uliooza, lakini hakuna anayepiga kelele kwa nguvu ya kutosha.

Ni wakati wa kufanya mabadiliko, na hilo halitafanikiwa kama sote tutaendelea kufumbia macho uozo uliopo.

Mpira wa Tanzania unahitaji mabadiliko ya kweli—na sasa ndiyo wakati wa kufanya hivyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad