Web

Siku Chache Kabla Mechi na Yanga, Tabora Yafichua Kuwafukuza Kocha na Kipa Kisa Tuhuma za Hongo




Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mheshimiwa Paul Chacha ikiwa zimebaki siku chache kabla ya kukutana na Yanga, amefichua kuwa klabu hiyo imemuondoa kocha na mlinda mlango wao kwa tuhuma za kuihujumu klabu hiyo.


Akizungumza kupitia kipindi cha Game Plan cha EFM Jumapili ya machi 30, 2025, Mhe Paul Chacha alisema kuwa yupo imara katika kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa klabuni.

Huku akikiri kumuondoa mlinda mlango wao, Hussein Masalanga baada ya kubaini kuwa alikuwa anahusika kwenye kuihujumu klabu ya Tabora United. Ambapo baada ya kupata vithibitisho alichukua uamuzi huo mara moja.

Mbali na Hussein Masala, Mhe Paul Chacha alikiri kumuondoa kocha mkuu wa Tabora United, Anicet Kiazayidi baada ya kugundua analikuwa anahusika pia kwenye kuhujumu maendeleo ya klabu hiyo kwenye mpira nchini.


Jambo lililomfanya aweke wazi kuwa yupo imara na muda wowote akigundua kuwepo kwa mchezaji au kiongozi ambaye anaihujumu Tabora United atamuondoa haraka mara baada ya kuthibitisha suala hilo.


Kauli za Mhe Paul Chacha zimeibua mjadala mkubwa, huku zikionesha wazi kuwa kama kuna ukweli kuhusu kile anachokisema ni wazi kuwa mpira wa Tanzania bado una safari ndefu kwani hongo si suala zuri kwenye soka.

Chanzo: EFM Tanzania (IG)


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad