Web

Sikukuu ya Eid El-Fitri ni Tarehe 31 March au 01 April 2025

Top Post Ad




Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) limetoa taarifa kwa Waislamu na Wananchi wote kwa ujumla kuwa Sikukuu ya Eid El-Fitri Itakuwa March 31,2025 au April 01,2025 kutegemea mwandamo wa mwezi.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu BAKWATA, Alhaj Nuhu Mruma imesema sherehe za Eid El-Fitri kitaifa kwa mwaka huu zitafanyika Mkoa wa Dar es salaam, swala ya Eid itaswaliwa katika Msikiti wa Mfalme Mohamed VI BAKWATA Makao Makuu Kinondoni kuanzia saa 1.30 asubuhi na kufuatiwa na Baraza la Eid litakalofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere kuanzia saa 09.00 mchana Inshallah, Mgeni rasmi katika Baraza la Eid atakuwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

“Kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania Mh. Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Dr. Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally Mbwana anawatakia Swaumu njema katika kumi la mwisho la mwezi Mtukufu wa Ramadhani na maandalizi mema ya Sikukuu ya Eid B-Fitri”

“Tunaomba Waislamu wote kuhudhuria kwenye Ukumbi kwa wingi na kwa wakati, Wabillahi Tawfiq”

Below Post Ad

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.