Nimefatilia mijadala mingi sana kuelekea dabi ya kariakoo wengi wanaipa nafasi kubwa Simba ya kufanya vizuri kuelekea kwenye mchezo huo na nilipojaribu kuhoji kuhusu sababu waliniambia kuwa Simba yupo vizuri sana.
Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini Yanga anaenda kupoteza mchezo wa dabi kwa sababu zifuatazo.
1. Yanga ndo timu ambayo ina safu bora ya ushambuliaji ile front three yao kule mbele ya Dube, Pacome na Mzize ni safu bora kuliko safu yoyote kwenye ligi kuu, fact ni kwamba ndo safu yenye magoli mengi kwa ujumla.
2.Yanga ndo timu yenye viungo wengi hatari wanaocheza eneo la kiungo sio dhidi ya Simba tu ni ligi kiujumla, Aziz, Aucho, Mudathir au Duke, na wengine wengi bado wanafanya vizuri lakini pia Yanga ndo timu ambayo inaongoza kwa kutengeneza nafasi nyingi mno wakiwa uwanjani.
3.Ukiangalia record za hivi karibuni Yanga amekuwa anafanya vizuri sana kwenye Dabi kuliko Simba hivyo bado kwenye Dabi ya jumamosi Yanga anaingia kama timu ya kwanza dhidi ya Simba.
4.Hata ukiangalia hiyo current perfomance bado Yanga anafanya vizuri na kikosi alichokuwa nacho kina huo uwezo wa kupambania ubingwa na kikashinda.
Nb; Simba anaweza kushinda hiyo mechi ila kwangu mimi Yanga ndo timu ya kwanza kuelekea mchezo huo.