Web

Simba Yasusia Mechi ya Derby ya Kariakoo Dhidi ya Yanga, Watoa Taarifa Hii

Simba Yasusia Mechi ya Derby ya Kariakoo Dhidi ya Yanga, Watoa Taarifa Hii



Klabu ya Soka ya imetangaza kususia kucheza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Wananchi, Young Africans Sc uliopangwa kuchezwa leo Machi 8, 2025 majira ya saa 1:15 usiku kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Taarifa ya leo Machi 8, 2025 iliyotolewa na klabu hiyo imebainisha kuwa sababu ya kufikia uamuzi huo ni kutokana na kunyimwa haki ya kufanya mazoezi kwenye uwanja wa mchezo muda tarajiwa wa mechi ambayo ni matakwa ya kikanuni.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Mabaunsa wa Klabu ya Yanga walivamia Msafara wa Simba huku wakifanya vurugu na kukizua Msafara wa Simba Sc kuingia uwanjani kufanya mazoezi kinyume na kifungu cha 17(45) chaa Kanuni za Ligi Kuu Bara, kinachosema “Timu Mgeni ina haki ya kufanya mazoezi kwenye uwanja wa mechi angalau mara moja kabla ya siku ya mechi katika muda tarajiwa wa mchezo husika.”



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad