KUTOKA BENJAMIN MKAPA MUDA HUU
Kikosi cha Simba kimefika katika Uwanja wa Benjami Mkapa lakini kimezuiliwa kuingia ndani ya uwanja huo na watu wanaodaiwa kuwa ni Makomandoo wa Yanga.
Kesho saa 1:00 usiku Yanga wataialika Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu na leo ilipaswa kuwa siku ya mwisho kwa wawili hao kufanya mazoezi ya mwisho katika uwanja ambao utatumika katika mchezo huo hapo kesho.