Presha ya sakata la kuhakikisha kwa dabi ya kariakoo linazidi kupanda ikiwa siku ya leo Alhamisi tarehe 27 Machi, ndio siku ya kikao cha maamuzi juu ya sakata hili ambacho kinakaliwa na viongozi wa serikali wakiwakilishwa na waziri wa habari, utamaduni sanaa na michezo Profesa Palamaganda Kabudi, wawakilishi wa Simba Sc, Yanga Sc, bodi ya ligi pamoja na TFF.
Taarifa za awali kutoka katika vyanzo mbalimbali vya habari za michezo nchini Tanzania zinaeleza kwamba wawakilishi kutoka pande zote wamewasili kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kwaajili ya kikao hicho isipokiwa wawakilishi kutoka Simba Sc ambao wao wamepangiwa muda wao wa kwenda.
Taarifa za kina kabisa kutoka vyanzo vya habari za michezo nchini Tanzania zinaeleza kwamba Simba Sc wataenda kwenye kikao hicho mchana mara baada ya wawakilishi wa Yanga Sc kumalizana na viongozi wa serikali.
Tafsiri rahisi ni kwamba kikao hicho kimegawanywa katika awamu mbili ambapo Yanga Sc wataanza kufanya kikao na baada ya kumaliza na baada ya hapo viongozi wa Simba Sc wataingia ili kusikilizwa na viongozi hao wa serikali.
Sambamba na taarifa hiyo, kuna taarifa nyingine inaeleza kwamba baadhi ya mashabiki na wanachama wa klabu ya Yanga Sc wamefika katika eneo la tukio ili kupinga kikao hicho kwa sababu wanaamini kwamba hakitakuwa na maslahi kwa upande wao.
Mashabiki hao wameandamana nje ya geti la uwanja wa Benjamin Mkapa na wanashinikiza kwamba kwamba msimamo wao ni uleule hawana mpango wa kucheza mchezo mwingine na hivyo basi viongozi wao walioenda kwa niaba ya klabu yao wanapaswa kusimamia msimamo wa klabu hiyo.
Wawakilishi wa Yanga Sc katika kikao hicho wakiongozwa na Rais wa klabu ya Yanga Sc Eng. Hersi Said wameweka wazi kwamba msimamo wao ni uleule kwamba hawachezi tena mchezo mwingine wa dabi ya kariakoo hata kama viongozi wa serikali watataka mchezo ule urudiwe.
Kikao bado hakijatoa maamuzi ya mwisho ya sakata hilo na wadau wa soka nchini Tanzania wanaendelea kusubiri maamuzi hayo ili kujua hatma ya mchezo huo kama utarudiwa au viongozi watafuata matakwa ya Yanga Sc ambao wameweka wazi kwamba hawana mpango wa kucheza tena.
Chanzo: Ayoma Tv, nassib mkomwa,Opera News