Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limekanusha taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii inayosema “WEZI WAIBA BASI LA POLISI MKOANI MBEYA” na kuiomba jamii kupuuza taarifa hiyo kwani hakuna tukio kama hilo mkoani Mbeya.
Taarifa ya leo Machi 17, 2025 iliyotolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mbeya imebainisha kuwa Jeshi la Polisi Mkoani humo halina basi lenye namba PT 4037 kama zinavyosomeka kwenye picha mnato iliyoambatishwa kwenye taarifa hiyo.
“Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na uchunguzi wa kuwabaini waliohusika na utoaji wa taarifa hiyo ya uzushi na kuleta taharuki kwa jamii ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi yao.”——imesema taarifa hiyo