Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Juma Mwapachu amefariki dunia leo Machi 28, 2025.
Enzi za uhai wake Balozi Juma Mwapachu pia aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, katika mashirika ya umma, sekta binafsi na kwenye asasi za kiraia nchini Tanzania, Kikanda na Kimataifa.