Kwanye hii miaka ya hivi karibuni ukimuondoa Aishi Manula aliyechukua tuzo ya mlinda lango bora back to back ana tuzo 6+ za ligi, ameivusha Simba bora kwenye michuano ya Caf, Afcon timu ya Taifa.
Feisal Salumu mchezaji mwingine mwenye mwendelezo wa ubora wake kwa miaka 4+ mfululizo bila kushuka Alicheza akiwa Yanga akachukua tuzo binafsi za kutosha ubingwa wa Yanga,
Feisal akajiunga Azam timu iliyopo kwenya kivuko cha kuingia kwenye timu kubwa kimafanikio Feisal anaibeba timu mabegani, kama kiungo kuingia kwenye orodha wa washambuliaji wawili bora sio kawaida, Kiungo bora kitakwimu na uwezo hakubahatisha ndiyo maana namba zinaendelea mpaka msimu huu.
Mtazame kwa sasa Clement Mzize alicheza mbele ya Mayele, anacheza mbele ya Msonda, Dube, Pacome na Chama, Guede kamkimbia.
Kila mwalimu anaekuja Yanga anamtumia anafunga anachezesha timu na anasaidia ulinzi anacheza kama mshambuliaji winga na kuna muda anashuka chini kama beki namba zake zinaongezeka kila msimu,
Warejee Simba na mbavu zao zote mbeli Kapombe + Hussen ukiulizwa nani aondoke pale Simba kati ya hawa wawili kila mtu atakuuliza kuna mafanikio yeyote ya Simba kwa zaidi ya miaka 10 utayataja bila kuzihusianisha hizi mbavu mbili za ulizi ?
Pale England waandishi wa habari wanatajwa kuwa sehemu kubwa ya kuwalinda wachezaji wao, kuna nyakati kwetu mchezaji bora ndiye anasimangwa zaidi kisa utani wa jadi na mambo mengine yasiyo ya muhimu.
unajiuliza kukosa muendelezo kwa wachezaji wazawa shida ipo wapi ????
@cheyolutenganotz
@bongotzfm