Web

Ulaya Yasimama na Zelenskyy, Aondoka Marekani Kwa Hasira



Ndege iliyombeba Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy imeondoka nchini Marekani na kuelekea London nchini Uingereza ambako Zelenskyy anatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Ulaya pamoja na Viongozi NATO kesho March 02,2025 huku Wanadiplomasia wakisema mkutano huo ni muhimu zaidi Barani Ulaya tangu vita vya pili vya Dunia.

Zelensky ameondoka Marekani baada ya jana February 28,2025 kuondoka Ikulu ya Marekani kwa hasira baada ya kuzozana na Trump na Timu yake mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu mjadala wa namna bora ya kumaliza vita ya Ukraine na Urusi.

Viongozi mbalimbali wa Ulaya wamesikitishwa na kitendo kilichofanywa na Marekani kwa Zelenskyy na kuahidi kusimama nae pamoja ambapo kesho Viongozi wa karibu Nchi zote za Ulaya watakutana kujadili jinsi ya kuitafuta amani na kumaliza vita ya Ukraine na Urusi bila kumkandamiza Zelensky, tayari Waziri Mkuu wa Poland ameandika mtandaoni akimwambia Zelenskyy kwamba “Haupo pekee yako”

Kwa upande wake Marekani chini ya utawala wa Rais Donald Trump tayari imetangaza kuwa haitoendelea tena kuisaidia Ukraine kifedha wala silaha za kivita kwasababu kipaumbele cha Marekani ni majadiliano ya amani na kumaliza vita ya Ukraine na Urusi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad