Web

Utajiri wa Elon Musk Waporomoka Baada ya Kujiingiza Katika Siasa za Marekani

 

Utajiri wa Elon Musk Waporomoka Baada ya Kujiingiza Katika Siasa za Marekani

Utajiri wa #ElonMusk umeshuka kwa zaidi ya dola bilioni 144 tangu Desemba, huku thamani ya hisa za Tesla ikishuka kwa 15% Machi 10, kutokana na wasiwasi wa wawekezaji kuhusu sera za ushuru za Trump. Hata hivyo, kufikia Machi 12, hisa zilikuwa zimepanda tena kwa 8.35%.


Wachambuzi wanadai kuwa kuhusika kwa Musk katika siasa, ikiwa ni pamoja na uongozi wake katika Idara ya Ufanisi wa Serikali ya White House, kumeteteresha chapa ya #Tesla na kuathiri masoko yake kimataifa. Mbali na hilo, #SpaceX imekumbwa na matatizo kufuatia uzinduzi wa majaribio ulioshindwa mara mbili, huku jaji wa shirikisho akiamuru idara yake kuweka rekodi wazi kwa umma.


Musk alijibu kuporomoka kwa hisa kwa kusema kila kitu kitakuwa sawa. Wakati huo huo, Trump alimuunga mkono kwa kuahidi kununua Tesla kama njia ya kupinga kampeni za kususia kampuni hiyo. Hata hivyo, wachambuzi wa soko wanamkosoa Musk kwa kutoonekana kwenye shughuli za Tesla, wakimtaka ashughulikie matatizo ya kampuni badala ya siasa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad