Sakata la M23 waasi wanao isumbua Kongo laendelea Kupata Suluhu kutoka Kwa Wakongo wazalendo. Vijana wa Kongo wameamua kuingia msituni wenyewe kukabiliana na kikundi Cha waasi Cha M23.
Waasi hao walivamia mashariki ya Kongo katika mji wa Goma na kufanya Kila aina ya uchafu. Kwa mujibu wa taarifa ambazo zilikuwa zinaripotiwa na vyombo mbalimbali vya Habari vilisema Raia wasio na hatia wanaendelea kupoteza maisha, wanabakwa, kupora Mali zao na mengine mengi kinyume na haki za Binadamu.
Licha ya ghadhabu zote ambazo raia walikuwa au wanaendelea kuzipata kutoka Kwa M23 Rais Felix Tshisekedi alikosa kabisa utatuzi wa suluhusho ilifika hatua alienda mpaka Chad kukutana na Rais wa nchi hiyo kuomba msaada.
Kitendo ambacho Wakongo hawakupendezwa nacho hivyo wakaamua kujikusanya kama kikundi kinacho fahamika jeshi la akiba au Wazalendo na kuanza kupambana na M23.
Baada ya raia kuonyesha moyo wa kutaka kupambana Rais Felix Tshisekedi aliamua kuungana nao Kisha akamteua Generali Yakutuba kutoa mafunzo Kwa vijana Wazalendo.
Felix Tshisekedi alichukua uamuzi wa kumteua Generali Yakutuba ambaye kiasili siyo Mkongoman ni Mtutsi kwa sababu ndani ya jeshi la Kongo kulikuwa na wasaliti ambao walikuwa wanavujisha mpaka ramani ya kivita.
Jambo ambalo lilipelekea Wanajeshi wengi wa Kongo kupoteza maisha. Hivyo Generali Yakutuba aliaminiwa na Felix Tshisekedi nakupewa kazi hiyo ya kuwanoa vijana huku akiacha askari ambao walikuwa na dalili za usaliti.
Tukio la Kuteswa Vikali Na Kuuawa Kwa M23 Na Wazalendo
M23 katika harakati za kutaka kumpindua Felix Tshisekedi walianza kuteka eneo la Goma wakatoka wakaenda Nyabibwe na Bukavu, walipofika eneo Moja linaitwa Fise ndio chozi lao la damu lilianzia hapo.
Walipo fika Fise walikita raia ambao walianza kiwashangalia M23, bila kujua ni mtego kwani vijana Wazalendo chini ya Generali Yakutuba walikuwa wamewatega katika eneo hilo ambalo lilikuwa kama kivuko Cha M23 kwenda Kinshasa kumpindua Felix Tshisekedi.
Hilo ndio eneo ambalo lilikuwa kama kaburi Kwa waasi wa M23 kwani wamepigwa na kuuawa vibaya sana na vijana Wazalendo.
Baadhi ya watu wamehoji kwamba Kongo ni nchi ambayo inasifikana kuwa na jeshi imara. Sasa inakuwaje jeshi la nchi lishindwe kupigana na M23 huku jeshi la akiba au Wazalendo wafanikiwe?.
Hapa ndipo utagundua kwamba jeshi hilo limejawa na wasaliti ambao wanauza taarifa Kwa waasi wa M23.