Yanga SC imetoa siku za mapumziko kwa wachezaji wake baada ya mchezo wa jana dhidi ya Coastal Union. Kikosi cha Young Africans kitarajea mazoezi siku ya Jumatano Machi 29 kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Tabora United utakaopigwa April 1 pale Tabora.
Wananchi, Young Africans SC wametinga hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho la CRDB kufuatia ushindi wa 3-1 dhidi ya Wanamangushi, Coastal Union katika uwanja wa KMC Complex Dar es Salaam
Young Africans itachukua na Songea united kwenye hatua inayofuata ya michuano hiyo. Kulingana na taarifa tulizozipata hivi sasa, Maxi Nzengele alifunga bao katika dakika ya 2 na 15. Naye Mzize dakika ya 21.
Simba SC watakutana na Bigman FC kwenye hatua ya 16 bora. Naye Tabora united atakutana na Kagera Sugar. Mashujaa FC watapatana na Pamba Jiji FC. Naye Singida BS watacheza dhidi ya KMC. Mwisho JKT Tanzania watapatana na Mbeya Kwanza. Mbeya City dhidi ya Mtibwa sugar. Mwisho Stand United watachuana na Giraffe Academy.