Web

Waliosema Kuwa Papa Francis Kafariki Waumbuka, Hii Hapa Picha Akiwa Kapata Nafuu

Waliosema Kuwa Papa Francis Kafariki Waumbuka, Hii Hapa Picha Akiwa Kapata Nafuu

Waliosema Kuwa Papa Francis Kafariki Waumbuka, Hii Hapa Picha Akiwa Kapata Nafuu

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis, ameonekana kwenye picha ya kwanza tangu alipolazwa Hospitalini mwezi mmoja uliopita.

Picha hiyo ambayo imetolewa na Vatican inamuonesha Papa akiwa amekaa kwenye kiti cha magurudumu mbele ya madhabahu kwenye Kanisa moja katika Hospitali ya Gemelli ya Rome, ambako amekuwa akipata nafuu kutokana na kuugua Nimonia.

Katika ujumbe wake alioutoa jana Jumapili, Papa alisema amepitia kipindi cha majaribio alipokuwa akiwashukuru Watu wanaomtakia mema kwa maombi yao, na kuombea amani katika nchi zilizoathirika na vita.

Jana ilikuwa ni Jumapili ya tano mfululizo ambayo Papa hakuhudhuria Kanisani, Vatican imesema vipimo vya X-ray vimethibitisha kuimarika kwa afya yake lakini bado anahitaji matibabu ya Hospitali.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad