Mashambulizi dhidi ya vituo vya Tesla yameongezeka baada ya #ElonMusk kushirikiana na utawala wa #Trump kwenye Idara ya Ufanisi wa Serikali (#DOGE), ambayo imepunguza matumizi makubwa ya serikali.
Miji kama Portland na Seattle imeathirika zaidi, huku magari ya Tesla, vituo vya kuchaji, na stoo za magari vikilengwa. Kwenye shambulio moja #LasVegas, magari kadhaa yaliwashwa moto na neno "#resist" likaandikwa kwenye jengo.
Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Pam Bondi, alisema watu watatu waliokamatwa kwa mashambulizi hayo wanakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 20 kwa ugaidi wa ndani.
Trump alitumia #TruthSocial kutangaza kuwa wahusika wanapaswa kufungwa kwa miaka 20 na kupendekeza wafungwe katika magereza ya #ElSalvador, akiyataja mashambulizi hayo kama ugaidi wa ndani. Alisisitiza kuwa Tesla ni "kampuni kubwa ya Marekani" na hata kununua gari lake la #Tesla kuonyesha uungaji mkono.