Wanaanga wanne wakiwemo Wanaanga wawili wa Shirika la Marekani la Sayansi na Teknolojia ya Angani (NASA), hatimaye wamerudi duniani usiku wa kuamkia leo March 19,2025 baada ya kukwama angani kwa miezi tisa.
Wanaanga hao ambao ni Butch Wilmore na Suni Williams pamoja na Mmarekani mwenzao Nick Hague na Wanaanga wa Urusi Aleksandr Gorbunov walitua baharini huko Florida huku wakishangiliwa na kundi la Watu.
Wanaanga hao wanne waliondoka duniani mwezi Juni mwaka jana katika safari ya kwenda angani kwa siku chache tu ila chombo kilichowabeba kilipata matatizo ya kiufundi na kudaiwa kuwa hakiko salama kuwarejesha duniani na kikaishia kurudi kitupu na hivyo walisalia angani kwa miezi tisa.
Misheni nyingi za anga huchukua takribani miezi sita, hivyo kwao kukaa zaidi ya miezi tisa kwenye kituo cha anga (ISS) ni jambo lisilo la kawaida, hasa kwakuwa walitarajia kukaa kwa siku nane tu kabla ya dharura kutokea, NASA imesema Watu hao wakiwa angani NASA ilipeleka vifaa vya anga kwa safari zaidi ya mbili vikiwa na chakula, maji, nguo na oksijeni kwa ajili ya kuwafanya waendelee kuishi na kusema Watu hao wakiwa angani walifanya tafiti mbalimbali ikiwemo uchunguzi wa jinsi mimea inavyokua angani, kufuatilia jinsi mwili wa binadamu unavyokabiliana na hali ya kutokuwa na uzito, na hata jinsi ya kupanda chakula.