Story ya Aishi Manula ilianza kubadilika baada ya kufungwq bao 5 na Yanga SC, yes pale skendo za kuuza mechi na wachezaji wengine zikaanza, Zile ni shutuma hivyo alitakiwa kutulia tu
Nakumbuka Manula alikua Majeruhi kwa muda mrefu Sana, na Ile mechi ya Yanga hakutakiwa kucheza lakini akakubali kucheza chini ya Robertinho, inawezekana ndio maamuzi anayoyajutia zaidi mpaka sasa
Manula akaanza kuonyesha kiburi na hata kuomba kuondoka, sasa hapa ni jeuri ambayo haisaidii ikiwa Ana mkataba na klabu yake,. Viongozi wa Simba wakamuongezea mkataba Ayoub Lakhred na Kumsajili Camara
Dili la Feisal kwenda Simba Sc likafa rasmi na wao wakavunja mpango wa kumpeleka Manula Azam FC, Manula hakupenda maana alitamani Sana kuondoka Simba Sc, wao wakmwambia aripoti kambini lakini hakuonekana hapo utakumbuka ata Simba day hakutambulishwa
Viongozi wakamwambia kijana una mkataba na timu unatakiwa kurudi, na hapo Imani ikaisha kabisa, ikabaki tu kua huyu atabaki Simba na atasugua benchi
Mpaka leo Manula hatupo kwenye headlins za magazeti tena, " huwezi kushindana na TAASISI"
.